|
|
Monday, 06 September 2010 10:36 |
|

|
|
Kocha wa timu ya Algeria Rabah Saâdane ameamua kumwaga manyanga kibarua chake kufauatia matokeo mabaya ya timu yake dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania. Mchezo huo wa AFCON -2012 ambao ulichezwa usiku wa kuamkia jumamosi wiki iliyopita katika uwanja wa Tchaker mjini Blida ulishuhudia Timu ya Algeria ikilazimishwa sare ya bao 1-1 ambapo Stars ndiyo waliokuwa wa kwanza kujipatia bao dakika ya 32 kupitia kwa Abdi Kassim kwa njia ya adhabu ndogo baada ya mshambuliaji wa Stars Mrisho Ngasa kufanyiwa madhambi na mabeki wa Algeria. Algeria waliweza sawazisha bao hilo dakika ya 45 baada ya Adlane Guedioura kuachia mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Stars Shaaban Kado.
Hata hivyo chama cha soka cha Algeria (AFA) kupitia kwa Mohamed Raouraou kimemshukuru Rabah Saâdane kwa mchango wake aliojitolea katika kipindi cha miaka mitatu aliyokuwapo kwenye timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuweza kuifanikisha timu kushiriki kombe la Dunia Afrika kusini.
|
 |
ALGERIA NATIONAL COACH RABAH SAADANE RESIGN
Algiers – National Coach Rabah Saâdane resigned from his office, less than 24 hours after the team’s disappointing performance Friday against Tanzania (1-1) at Tchaker Stadium in Blida, as part of the 1st day of African Nations Cup- 2012 qualifier, Algerian FA said Saturday. Rabah Saâdane decision has been approved by the Algerian Football Association (FA) Mohamed Raouraoua who was keen to thank the manager and pay him tribute for the excellent work accomplished, the same source added. Saadane took charge three years ago and steered Algeria to their first World Cup in 24 years in South Africa. Under him, Algeria reached semi-finals of the African Cup of Nations in 2010 in Angola.
|
|

|
| |
|
|
|
Thursday, 02 September 2010 11:53 |
|

|
|
Katika jitihada za kuutangaza mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa kampuni ya Exotic Flight Services Limited kwa kushirikiana na shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania (PST) wameandaa pambano linalotarajiwa kufanyika jijini Dar Es Salaam Desemba 9 katika uwanja wa Taifa.
Pambano hilo ambalo litawakutanisha mabondia Hechor Camacho Junior toka Puerto Rico na Roy Jones Junior toka nchini Marekani linatarajiwa kuwa kiburudisho tosha katika Afrika mashariki kwani Bingwa wa zamani wa ndondi uzani wa juu Duniani , Mike Tyson na mwanamuziki Britney Spears wanatarajiwa kuwapo katika kusherehesha mchezo huo.
Mbali na mabondia hao watakaokuwa wakiwania mkanda wa shirikisho la ndondi la UBO, uzani wa Super- middle, mabondia wazawa nao watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao. |
 |
|
TYSON TO BE IN DAR FOR BIG FIGHT SHOW.
In the strategy to expose Tanzania boxing, the Tanzania boxing federation in collaboration with Exoting Flight Private Jet Services has organized Big Fight that will involve two Boxing Superstars Roy Jones Jr (US) and Hector Camacho (Puerto Rico) around December 9 in Dar es Salaam at the National Stadium.
The fight is expected to include legendary Mike Tyson as being the ring announcer while the prominent American musician, Britney Spear will color the bout.
Apart from the foreign fighter who is going to compete for the UBO title of 12 Round fight; local boxers will also capitalize this opportunity to be known in international level.
|
|

|
| |
|
|
Saturday, 28 August 2010 12:23 |
 |
|
Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, klabu ya Chelsea leo jumamosi wanakutana na timu ya Stoke city katika mfululizo wa ligi ya Barclays.
Chelsea wenye rekodi nzuri mpaka sasa katika msimamo wa ligi hiyo wanaongoza wakiwa na point sita na magoli kibao baada ya kuzishushia mvua ya magoli sita kila mmjo timu za West Bromwich na Wigan Athletic.
Wapenzi wengi wa ligi ya Uingereza hasa mashabiki wa Chelsea leo watakuwa na hamu kubwa kuona kama timu yao itaendeleza wimbi la ushindi mkubwa wa mabao mchezo utakaopigwa katika dimba la Stanford Bridge jijini London.
Mechi zingine zitakazo pigwa leo ni Blackburn vs Arsenal, Blackpool vs Fulham, Tottenham vs Wigan, Wolvehampton vs Newcastle, wakati Man United dhidi ya West Ham. Kwa maelezo zaidi fuatilia Kabumbu Halisi kupitia nipe5.com.
|
 |
|
WILL CHELSEA CONTINUES TO RELISH ITS RECORD?
The defending champion for English premier league, Chelsea today is going to face Stoke city at its home ground pitch Stanford Bridge stadium. Being at the top in the Barclays premier ranking chat, Chelsea have already scored twelve goals in two matches after thrashing West Bromwich and Wigan Athletic with six goals to each.
Many Chelsea’s fans around world are waiting the final wrestle to see how much scores will their club going to obtain in today’s match.
Other fixture for today’s matches include Blackburn vs Arsenal, Blackpool vs Fulham, Tottenham vs Wigan, Wolvehampton vs Newcastle, and Man United against West Ham.
You can get more information through kabumbu halisi link at nipe5.com.
|
| |
|
|
|
Friday, 27 August 2010 12:00 |
 |
|
Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limekipa haki kituo cha Star Tv kurusha matangazo ya michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka huu.
Akizungumza jana, ofisa habari wa TFF, Florian Kaijage, alisema kuwa kamati ya utendaji ya TFF iliyokutana juzi ilipitia majina ya makampuni yaliyoomba kurusha matangazo hayo na kuamua kuipa Sahara Media ambayo inamiriki kituo cha Star Tv.
Vituo vingine vilivyokuwa vikiomba dhamana hiyo kwa TFF ni pamoja na Indepent Television (ITV), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Kampuni hiyo ya Sahara italazimika kulipa kitita cha shilingi milioni 140 ili kupata fursa hiyo.
|
|

|
|
STAR TELEVISION TO BROADCAST TANZANIA LEAGUE.
Tanzania Football Federation (TFF) has given Sahara Media rights to broadcast Tanzania premier league in this Vodacom league season.
The body’s information officer, Florian Kaijage said that there was various local stations that competed for the tender but non meet the standard settled, except the Star Television which come to win the bid.
Star will be required to pay 140 millions so as to be legitimate television to broadcast the show. |
| |
|
|
Tuesday, 24 August 2010 11:18 |
|

|
|
Akiwa kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya ngumi za ridhaa huko Lugogo, Kampala mnamo December 9, 1974 , Idd Amin aliushangaza umati wa watu waliokuwapo kwenye uzinduzi huo baada ya kuamrisha acheze pambano na Mwenyekiti wa mchezo wa Ngumi bwana Peter Seruwagi.
Katika pambano hilo Amin alimchakaza mpinzani wake kwa knock-out huku akiwa amevaa tai. Seruwaga akiongea na jarida la The East African alikaririwa akisema kuwa alimpa mwanya wa kushinda pambano hilo Amin Kutokana na ukweli kuwa Kiongozi huyo alikuwa anataka kulipiza kisasi kutokana na yeye kumshinda kwenye pambano lao miaka kumi na sita iliyopita walipokuwa chuo.
Amin katika ujana wake ameshakuwa bingwa wa uzito wa juu nchini Uganda kuanzia mwaka 1955 mpaka 1959 kabla ya rekodi yake kuchafuliwa na Seruwaga mwaka 1958.
|
|

|
|
IDD AMIN BOXER OF THE YEAR.
Being a special guest in the opening for sixth All Africa Amateur Boxing Championships in Lugogo, Kampala on December 9, 1974, Idd Amin declared that he would open the championships by boxing with Peter Seruwagi ( The Ugandan national coach by that time) in a curtain raiser. The Amin vs Seruwagi match was not scheduled in the event before but in Amin’s way of conducting affairs, that was no obstacle. Speaking with the East African Magazine Seruwagi said that the fight ended in a knock-out in favour of Amin.
It is said that Amin was the undefeated heavyweight champion from 1955 to 1959. But Seruwage floored him in a special fight in 1958. So, Amin was there for revenge.
|
| |
|
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>
|
|
Page 1 of 15 |