HOT & HAPPENING

Wanafunzi wafanya Vizuri katika Michezo Dar..

April 7, 2008

WANAFUNZI wa Taasisi ya Tanzania Sports Academy (TSA), ambayo inamiliki shule ya Sekondari ya Wining Spirit ya jijini Arusha, jana waling’ara katika mashindano ya Dar Coca Cola Half Marathon yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo ya kilomita 21, wanariadha kutoka mikoa mbalimbali walionekana kuzidiwa nguvu na washiriki kutoka Arusha walioshinda nafasi za juu.

Katika mbio hizo zilizoanza majira ya saa 12:00 asubuhi zikifunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Nkaya Bendera, washindi 10 bora kwa upande wa wanaume walitoka mkoaniArusha huku kwa upande wa wanawake nafasi tano zilichukuliwa pia na wanariadha kutoka mkoa huo.

You have no rights to add a new comment. May be you need to register on the site.

Latest Comments

People You may know!

Please login to be able to see the Content!