26 August 2010
![]() |
|
Mwanamuziki maarufu wa Uingereza, Alexandra Burke amekiri kwamba anahaha kusaka mchumba na kwamba amekuwa mnyonge sana kwa kuishi bila mwanaume. Alexandra pamoja na kusema hivyo alionya kwamba anatatizwa na suala zima la siri na uaminifu katika mapenzi baada ya aliyekuwa rafiki yake wa zamani wa kiume kuanika mambo yao ya ndani kwenye vyombo vya habari. Kutokana na ukweli huo, Alexandra anasema kwa sasa anajikuta akiwa njia panda na kuwa umaarufu na uwezo wake wa kifedha unamfanya akutane na wanaume walaghai wenye tamaa ya fedha. “Najisikia mnyonge kweli yaani kuna wakati hali yangu inakuwa mbaya, nimewahi kuwa katika mahusiano a wanaume wawili na wote waliniweka katika wakati mgumu kwa kukosa uaminifu, najua nina tatizo hilo na hapo ndipo ninapokuwa na wasiwasi wa kuingia katika mapenzi,”alisema. Alexandra alisema aliwahi kuwa na mahusiano na mtu ambaye alisoma naye cheke chea lakini baadaye alimgeuka na kuwa muongo:”Kama mtu wa aina hiyo anaweza kukudanganya basi kuna tabu kuamini mtu.” |
|
|
|
ALEXANDRA BURKE ON VERGE LONELINESS. Alexandra Burke, musician from Britain has revealed to the public that she is facing strong emotional after separation with his ex-boyfriend with whom they had been together for a long time. In elaborating her explanation, Burke said” I have come across a series of friendship, but none of them was sufficient to me, since most of the guys didn’t sympathy show true love to me. They were after my personality.” “Now am feed up with all these frustration, I need a guy who will show true concern to me”, she added.
|
















