05 May 2010
![]() |
|
Roboti mwenye miguu miwili sasa kutembea mwezini ifikapo mwaka 2015, hii imesemwa na kundi la makampuni mjini Japan , Roboti huyo atakuwa tofauti sana na roboti walio wahi kupelekwa mwezini hapo awali, kundi hilo limesema kwamba kitu cha kwanza ambacho roboti huyo atafanya ni pamoja na kuchora bendera ya Japani akiwa huko mwezini. Wachunguzi wamesema roboti mwenye kutumia matairi au Yule mwenye miguu mingi ndiye anayeweza kustahimili akiwa mwezini , ila ikaja kupingwa na Hideo Sugimoto raisi wa SOHLA(Space Oriented Higashiosaka Leading Association) akisema kwamba roboti anataweza kutembea kwa miguu miwili kama binadamu na italeta mantiki. Projekti hii itawagharimu kiasi cha dola milioni kumi ,kwani kumfanya roboti atembee kwa miguu miwili ni changamoto kubwa sana. |















